Skip to main content

New e-CMS system launching February 1, 2026 | Learn more

JAJI MKUU AFUNGUA MAFUNZO YA TATHIMINI YA MRADI WA MABORESHO YA MAHKAMA

2025-10-04 Zanzibar Judiciary
Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Khamis Ramadhani Abdalla, amesema uwepo wa Mafunzo kwa watendaji wa Mahkama wakiwemo Majaji, Mahakimu na Makadhi, utasaidia kuimarisha utendaji wa Mahkama na kuongeza ufanisi katika utoaji wa haki kwa wananchi.\r\n\r\nAkizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo kwa Majaji, Mahakimu na Makadhi kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Maboresho ya Mahkama (Zanzibar Judiciary Modernization Programme – Zi-JUMP), unaofadhiliwa na benki ya Dunia katika Hoteli ya The Residence, Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja.\r\n\r\nAidha alisema Mradi wa Maboresho ya Mahkama ni ushahidi wa dhamira ya dhati ya Mahakama ya Zanzibar katika kuimarisha upatikanaji wa haki kwa wananchi, na kuongeza uwazi, uwajibikaji, sambamba na kujenga mfumo wa Mahkama za kisasa unaoendana na kasi ya maendeleo ya dunia.\r\n\r\nJaji Mkuu alisema hadi sasa mafanikio kadhaa yamepatikana kupitia mradi huo ikiwemo Mafunzo mbali mbali kwa watumishi wa Mahkama, kuanza kwa kazi ya utengenezaji wa mfumo wa kusimamia mashauri kwa njia ya kielektroniki (ECMS) na uanzishwaji wa mfumo wa upimaji wa utendaji wa watumishi wa mahakama.\r\n\r\n “Ni wajibu wetu kama watumishi wa Mahakama kuhakikisha tunatekeleza majukumu yetu kwa uadilifu, uaminifu na kwa kuzingatia maadili ya kazi, maboresho haya si kwa ajili ya mfumo pekee, bali ni kwa ajili ya wananchi wanaotegemea kupata haki kwa wakati,” alisisitiza Mhe Jaji Mkuu\r\nNae Mratibu wa Mradi wa Zi-JUMP, Jaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar Mhe. Ibrahim Mzee Ibrahim, alisema mradi huo umekuwa kichocheo cha Mabadiliko chanya ndani ya Mahakama na utaongeza ari kwa watendaji.\r\n\r\nKwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Mahkama Zanzibar Mhe. Kai Bashir Mbarouk alisema mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa Zi-JUMP unaolenga kuboresha ufanisi wa utendaji wa Mahakama, kuongeza uwazi wa taarifa kwa umma na kujenga uwezo wa watumishi wa sekta ya sheria katika matumizi ya mifumo ya kisasa.\r\n\r\nAidha alisema Mafunzo hayo yatawawezesha Majaji na Mahakimu kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu mabadiliko yanayoendelea ndani ya Mahkama, hasa katika matumizi ya TEHAMA kama nyenzo ya kuongeza kasi na uwazi wa utoaji haki.