Skip to main content

New e-CMS system launching February 1, 2026 | Learn more

JAJI IBRAHIM AFUNGUA KIKAO CHA TATHIMINI YA MRADI WA MABORESHO YA MAHKAMA.

2025-10-18 Zanzibar Judiciary
Jaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar Mhe. Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim amesema Mradi wa Maboresho ya Mahkama ni ushahidi wa dhamira ya dhati ya Mahakama ya Zanzibar katika kuimarisha upatikanaji wa haki kwa wananchi, na kuongeza uwazi, uwajibikaji, sambamba na kujenga mfumo wa Mahkama za kisasa unaoendana na kasi ya maendeleo ya dunia.\r\n\r\nAkizungumza katika ufunguzi wa Kikao cha Tathimini ya mwaka mmoja wa utekelezaji wa Mradi wa Maboresho ya Mahkama (Zanzibar Judiciary Modernization Programme – Zi-JUMP), unaofadhiliwa na benki ya Dunia katika Hotel ya Golden Tulip\r\n\r\n Alisema ni wajibu wa watumishi wa Mahakama kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na kwa kuzingatia maadili ya kazi, maboresho haya si kwa ajili ya watumishi wa Mahkama pekee, bali ni kwa ajili ya wananchi wanaotegemea kupata haki kwa wakati.\r\n\r\nMradi huu wa maboresho ya Mahkama umebuniwa kwa lengo la kuboresha mazingira ya utoaji haki, kuimarisha matumizi ya teknolojia katika shughuli za Mahkama, kuongeza uwazi na uwajibikaji, pamoja na kuboresha uwezo wa watumishi wa Mahakama katika nyanja mbalimbali za kazi zao\r\n\r\nAkitaja mafaniko yaliyopatikana kwa kipindi cha mwaka mmoja ya utekelezaji wa maradi ni Mafunzo kwa watumishi wa Mahkama ambapo jumla ya watumishi 187 wamepatiwa mafunzo mbali mbali, kuanza kwa kazi ya kuunda mfumo wa kupokea mashauri kwa Njia ya kieletronic, kupungua kwa mrundikano wa mashauri Mahkamania\r\n\r\nkwa upande wake kaimu Mrajis wa Mahkama Kuu ya Zanzibar Mhe. Faraji Shomari Juma alisema Mradi umelenga kuleta mabadiliko katika utendaji ikiwemo uendeshaji wa kesi kupitia mfumo wa kielekronic. Jambo amabalo litawasaidia wafanyakazi wa kada mbalimbali, na kuongeza kuwa ni lazima kila mtendaji kwa mujibu wa kada zao apatiwe elimu kuhusu mradi huo ili iwe ni chachu ya mabadiliko katika Mahkama. \r\n\r\nNao baadhi ya washiriki wa kikao hicho walisema watahakikisha mafanikio yaliopatikana kupitia mradi huo yanaleta tija kwa kutatua changamoto zinazojitokeza kwa wakati na kuleta ufanisi katika utendaji wa kazi zao kwa mujibu wa sheria.