Skip to main content

New e-CMS system launching February 1, 2026 | Learn more

JAJI HAJI AFUNGA MAFUNZO YA MFUMO WA USIKILIZAJI WA MASHAURI KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

2026-01-03 Zanzibar Judiciary
JAJI HAJI AFUNGA MAFUNZO YA MFUMO WA USIKILIZAJI WA MASHAURI KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI\r\n\r\nJaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar Mhe. Haji Khamis Suleiman amesema uwepo wa mfumo wa usikilizaji wa mashauri kwa njia ya kielektroniki itakua ni chachu ya kuharakisha utoaji wa haki na kupunguza urundikaji wa mashauri mahkamani.\r\nAmeyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya siku tano ya majaribio ya mfumo wa usikilizaji wa mashauri kwa njia ya kielektroniki yaliyofanyika katika Hoteli ya Madinat Al Bahr iliyopo Mbweni Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.\r\nAmesema kuwa mfumo huo ni suluhisho la kuharakisha utendaji kazi wa vyombo vya sheria, kuboresha uwazi, na kuhakikisha haki inatolewa kwa wakati na kwa ufanisi zaidi.\r\nMhe. Jaji ameishauri Mahkama kujiweka tayari kwa kuwapatia watendaji wake huduma muhimu zinazokwenda sambamba na mfumo huo ikiwemo mtandao imara na wenye kasi pamoja na vitendea kazi vya kisasa ili mfumo huo utumike kama ulivyokusudiwa. \r\nMhe. Jaji pia amewashukuru washiriki wote kwa ushirikiano na juhudi walizozionesha katika kipindi chote cha mafunzo, na kuwataka kutumia ujuzi walioupata katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku, sambamba na kuwapongeza waundaji wa mfumo huo kwa kazi nzuri waliyoifanya, na kuwapongeza wawezeshaji na waratibu kwa kufanikisha mafunzo hayo kama ilivyokusudiwa.\r\nNao washiriki wa mafunzo hayo wameushukuru uongozi wa Mahkama kwa kuwapatia mafunzo juu ya mafumo huo na kutengeneza mfumo ambao utakua ni msaada mkubwa katika kuharakisha utoaji wa haki na utamfanya mtumiaji aweze kufungua shauri popote alipo duniani.\r\nMfumo wa usikilizaji wa mashauri kwa njia ya kielektroniki umetengezezwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia chini ya mradi wa Maboresho ya Mahkama (Zi-JUMP).