JAJI IBRAHIM AFUNGUA WARSHA YA KUJADILI MATOKEO YA UTAFITI WA CUS
2026-01-03
Zanzibar Judiciary
JAJI IBRAHIM AFUNGUA WARSHA YA KUJADILI MATOKEO YA UTAFITI WA CUS\r\n\r\nJaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar Mhe. Ibrahim Mzee Ibrahim amesema kuwa Mahkama ya Zanzibar itahakikisha kuwa inatoa haki kwa wananchi bila ya ubaguzi wa aina yoyote.\r\nWakati akifungua warsha ya siku mbili ya kujadili Matokea ya Utafiti wa Ridhaa ya Watumiaji wa Huduma za Mahkama inayofanyika katika Hoteli ya Madinat Al Bahr iliyopo Mbweni Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, amesema ipo haja matokea ya utafiti wa kufikishwa kwa wadau na jamii kwa ujumla ili waweze kuelewa kilichomo ndani ya utafiti huo.\r\n\r\nAidha, ameeleza kuwa tafiti mbalimbali zinazofanywa na Mahkama pamoja na mipango yake inakwenda sambamba na Dira Kuu ya maendeleo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (2050) ambayo imeeleza wazi kuwa lengo la Mahkama ni kuweka mfumo mzuri wa kushughulikia madai na kuharakisha uendeshaji wa kesi.\r\n\r\nNae, Mkurugenzi wa Mipango na Utafiti wa Mahkama ya Zanzibar Nd. Mohamed Salum amesema kufanya tafiti ni muhimu kwa sababu husaidia kwa asilimia kubwa katika kufanya maamuzi ya kiutendaji.\r\n\r\nAmefafanua kuwa utafiti umegusia katika maeneo zaidi ya 80 ambayo yamewekwa kwenye makundi makuu matano ambayo ni; huduma za mahkama, uwazi wa mahkama katika huduma zake, hadhi ya huduma zinazotolewa na mahkma, upatikanaji wa huduma zenyewe na utatuzi wa migogoro ya wanajamii wanaofungua kesi mahkamani.\r\n\r\nUtafiti wa Ridhaa ya Watumiaji wa Huduma za Mahkama (CUS) umefanyika kwa ufadhili wa Benki ya Dunia chini ya mradi wa Maboresho ya Mahkama (Zi-JUMP).