Skip to main content

New e-CMS system launching February 1, 2026 | Learn more

JAJI MKUU WA ZANZIBAR AKABIDHI VYETI KWA MAWAKILI NA MAVAKILI

2026-02-04 Zanzibar Judiciary
Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla amewataka Mawakili kutochanganya kazi yao na siasa kwani kufanya hivyo hupelekea kuchonganisha wananchi na Mahkama na kuwafanya wananchi kutokuwa na Imani na Mahkama kwa kile walichoelezwa na mawakili wao.\r\n\r\nAmeyasema hayo wakati akitunuku vyeti kwa Mawakili na Mavakili wapya hafla hiyo imefanyika katika Jengo la Mahkama Kuu Tunguu ikiwa ni miongo wa shughuli za kuadhimisha wiki ya Sheria Zanzibar.\r\n\r\nAidha alisema kuwa imefika wakati sasa kwa kutungwa kwa kanuni ambazo zitatenganisha wanasiasa kujishuhulisha na kazi za uwakili ili kurejesha heshima ya taaluma ya Sheria Zanzibar.\r\n\r\nVile vile Mhe. Jaji Mkuu aliwakumbusha kuwa taaluma ya uwakili ni dhamana kubwa kwa jamii. Mawakili ni walinzi wa haki, usawa na utawala wa sheria. Hivyo basi, ni wajibu wao kuitekeleza kazi yao kwa uadilifu, weledi na heshima kubwa kwa sheria na maadili ya taaluma zao.\r\n\r\nPia Mhe. Jaji Mkuu alitoa wito kwa Mawakili na Mavakili kutumia taaluma zao kuitumikia jamii, hususan makundi yenye uhitaji kama wanawake, watoto na watu wasio na uwezo wa kifedha. Haki si kwa wenye uwezo pekee, bali ni haki ya kila mmoja\r\n\r\nKwa upande wake, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Zanzibar, Nd. Shaaban Ramadhani Abdalla, amesema kuwa Serikali inaendelea kuthamini mchango wa mawakili na mavakili katika kusimamia haki na utawala wa sheria. \r\n\r\nAmeeleza kuwa taaluma walioipata mawakili na mavakili itasaidia kuimarisha uelewa wa kisheria, kuongeza weledi katika utoaji wa huduma za sheria na kupunguza changamoto katika uendeshaji wa mashauri. Aidha, amewataka kuzingatia maadili, sheria na kanuni katika utekelezaji wa majukumu yao.\r\n\r\nNae Rais wa Chama cha Mawakili Zanzibar, Wakili Joseph Shaaban Magazi, amewahimiza jifunza na kuendelea kujijengea uwezo kwani Sheria ni taaluma inayobadilika kila siku. Endeleeni kusoma, kushiriki mafunzo na kubadilishana uzoefu na wenzenu ili muweze kutoa huduma bora kwa wateja na kwa jamii kwa ujumla.\r\nJumla ya wamakili 57 na Mavakili 13 walitunukiwa vyeti vyao vya kuwa Mawakili na Mavakili.