Skip to main content

New e-CMS system launching February 1, 2026 | Learn more

MAHKAMA YA ZANZIBAR YAUNGA MKONO WANANCHI KUPITIA SHUGHULI ZA USAFI NA MSAADA KWA WENYE MAHITAJI MAALUM

2026-02-06 Zanzibar Judiciary
Mtendaji Mkuu wa Mahkama ya Zanzibar Mhe. Kai Bashir Mbarouk ameahidi kuwa Mahkama itaendelea kutoa misaada mbalimbali kwa watu wenye mahitaji maalum na wananchi kwa ujumla ili kuwa karibu na wananchi.\r\n \r\nAkizungumza wakati wa shughuli ya usafi wa mazingira na utoaji wa vifaa mbalimbali kwa wananchi wenye mahitaji maalum katika hospitali ya Wilaya Vitongoji-Pemba na Skuli ya Elimu Mjumuisho Maandalizi na Msingi iliyopo Pujini-Pemba, amesisitiza kuwa Mahkama ya Zanzibar imeendelea kuwa karibu na wananchi kwa kuunga mkono jitihada mbalimbali zinazolenga kuboresha maisha na ustawi wa jamii, kinyume na dhana iliyowepo kwa baadhi ya wananchi kuwa Mahkama ni taasisi inayohusika na masuala ya kisheria pekee.\r\n\r\nVile vile aliwaomba walimu wa Skuli ya Pujini kuwafundisha watoto wenye mahitaji maalum kama watoto wao wa kuzaa ili kujenga upendo baina yao na kuwafanya wajihisi kuwa wapo katika sehemu salama kwa mustakabali mzuri wa maisha yao.\r\n\r\nNae Dkt. Dhamana wa hospitali ya Wilaya Vitongoji-Pemba Dkt. Said Ismail Ali ameipongeza Mahkama ya Zanzibar kwa kuendelea kushirikiana na wananchi katika masuala ya kijamii na maendeleo, akieleza kuwa hatua hiyo inaonesha wazi dhamira ya Mahkama katika kuwaletea wananchi huduma jumuishi zinazogusa nyanja mbalimbali za maisha yao.\r\n\r\nAidha, ameiomba Mahkama ya Zanzibar kuendelea kushiriki na kuunga mkono shughuli zinazolenga kulinda afya, mazingira na haki za makundi yote ya kijamii, kama sehemu ya wajibu wake katika kujenga jamii yenye ustawi na maendeleo endelevu.\r\n\r\nNae Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Elimu Mjumuisho Maandalizi na Msingi iliyopo Pujini-Pemba Nd. Makame Hamad Makame wakati akipokea zawadi kwa niaba ya watoto wa skuli hiyo ameushukuru uongozi wa Mahkama kwa moyo wao wa imani kwa watoto wenye mahitaji maalum na kuiomba kuendelea kutoa misaada kama hiyo katika maeneo mengine nchini.\r\n\r\nShughuli ya usafi wa mazingira pamoja na utoaji wa vifaa kwa wenye mahitaji maalum imefanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Sheria Zanzibar.