Skip to main content

New e-CMS system launching July 1, 2026 | Learn more

KAIMU MTENDAJI MKUU WA MAHKAMA YA ZANZIBAR AFUNGUA MAFUNZO YA KULINDA HAKI ZA WATOTO

2026-06-12 Zanzibar Judiciary
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mahkama ya Zanzibar Ndugu Mohamed Salum Mohamed amesema kuwa Mahkama ina nafasi ya kipekee katika kuhakikisha kuwa kila mtoto anayefika katika mfumo wa utoaji haki anapata haki zake kwa mujibu wa sheria, kwa kuzingatia maslahi bora ya mtoto, utu wake.rnAmeyasema hayo wakati akifungua Mafunzo kwa Mahakimu na Makadhi katika kuelekea kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika ukumbi wa Mahkama Kuu TunguurnAidha alisema kuwa mafunzo haya yanalenga kuimarisha uelewa na uwezo wa watumishi wa Mahkama katika kushughulikia masuala yanayohusu watoto kwa weledi, huruma na kwa kuzingatia sheria za kitaifa na mikataba ya kimataifa inayolinda haki za mtoto.rn“Maadhimisho haya yanatukumbusha wajibu wetu wa kuhakikisha kuwa kila mtoto anapata haki zake za msingi, ikiwemo haki ya kulindwa, kusikilizwa, kuelimishwa na kupata huduma za haki bila ubaguzi wowote. Kwa mwaka 2026, kaulimbiu ya Siku ya Mtoto wa Afrika ni "Linda mtoto wa Afrika; mpe afya bora na maisha bila ya udhalilishaji", ikisisitiza umuhimu wa mazingira salama kwa maendeleo na ustawi wa Watoto”. Alisema ndugu Mohamed rnAlieleza kuwa Mafunzo haya kwa Mahakimu na Makadhi yamekuja wakati ambapo jamii inaendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali zinazowakabili watoto, ikiwemo ukatili, kutelekezwa, migogoro ya kifamilia na makosa yanayowahusisha watoto. Hivyo, ni muhimu kwa watendaji wa Mahkama kuendelea kuimarisha uelewa wao kuhusu sheria za mtoto, mbinu rafiki za kusikiliza mashauri yanayohusisha watoto na matumizi ya misingi ya haki za mtoto katika kufanya maamuzi.rnMaada mbali zimewasilishwa kwenye Mafunzo hayo zikiwemo Maslahi bora ya mtoto, Mzingira Rafiki kwa Mtoto na Ujumuishwaji wa jinsia katika mfumo wa haki.