Skip to main content

New e-CMS system launching July 1, 2026 | Learn more

MAKABIDHIANO YA MFUMO WA USAJILI NA UENDESHAJI WA MASHAURI KWA NJIA YA KIELETRONIK (e-CMS)

2026-06-16 Zanzibar Judiciary
Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe Khamis Ramdhan Abdalla, amesema kuwa Mfumo wa Usajili na Uendeshaji wa Mashauri kwa Njia ya kieletronik (e-CMS) utaanza kutumika rasmi kuanzia tarehe rasmi 1 Julai 2026, kwa Mahkama Kuu ya Zanzibar kwa Upende wa Unguja na Mahkama zote zilizokuwemo kwenye Mkoa wa Mjini Magharib, huku akiwataka wadau wote wa Mahkama na wananchi kwa ujumla kuwa tayari kuanza kutumia mfumo huo ili kuimarisha utoaji wa huduma za haki.\r\nMhe. Jaji Mkuu alitoa kauli hiyo wakati wa hafla ya makabidhiano ya Mfumo huo kutoka kwa wataalamu wa ujenzi wa mfumo kwenda kwa uongozi wa Mahkama ya Zanzibar, iliyofanyika tarehe 16 Juni, 2026 katika Mahkama Kuu Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja.\r\nAidha Mhe Jaji Mkuu amesema kuwa Makabidhiano ya mfumo huo ni utekelezaji wa dira ya Mahakama ya Zanzibar ya kujenga Mahkama za kisasa, zinazotoa huduma kwa ufanisi, uwazi na kwa wakati. Mfumo hu utaongeza kasi ya utoaji wa haki, kupunguza kupunguza mrudikano wa Mashauri Mahkamani.\r\n Mhe. Jaji Mkuu amemshukuru Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania, Mhe. Ibrahim Mzee Ibrahim, kwa mchango wake mkubwa katika usimamizi wa Mradi wa Maboresho ya Mahkama (Zi-JUMP), akieleza kuwa uongozi na usimamizi wake umechangia kwa kiasi kikubwa kufanikisha utekelezaji wa mradi huo. Aidha, aliwapongeza wajenzi wa mfumo wa e-CMS kwa kazi yao ya kitaalamu iliyowezesha kukamilika kwa mfumo wenye ufanisi mkubwa.\r\nKwa upande wake, mratibu mstaafu wa Mradi wa Zi-JUMP Mhe. Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim alisema kuwa katika hatua ya mwanzo mfumo huo utapokea na kushughulikia maombi mapya pekee, huku mashauri yote yaliyosajiliwa kabla ya kuanza kutumika kwa mfumo yakiendelea kusikilizwa kwa utaratibu wa kawaida hadi yatakapokamilika.\r\nAlifafanua kuwa mfumo huo umefikia takriban asilimia 94 ya utekelezaji na umeundwa ukiwa na vipengele 16 vitakavyowezesha matumizi yake kwa watumishi wa ndani ya Mahkama pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya haki.\r\nMfumo wa e-CMS ambao umefadhiliwa na Benkiy a Dunia kupitia mradi wa Maboresho ya Zi-JUMP umejengwa na Mahkama ya Zanzibar kwa ushirikiano na wataalamu kutoka taasisi mbalimbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ukiwa na lengo la kuboresha usajili, uendeshaji na usimamizi wa mashauri kwa kutumia teknolojia ya kidijitali na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za Mahkama.