Skip to main content

New e-CMS system launching February 1, 2026 | Learn more

JAJI MKUU WA ZANZIBAR AFUNGUA MAFUNZO WA MAJAJI NA MAHAKIMU KUHUSU UTATUZI WA MIGOGORO YA UCHAGUZI

2025-10-04 Zanzibar Judiciary
Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla amewataka Majaji na Mahakimu kuishughulikia Migogoro ya uchaguzi itakayoletwa katika Mahkama kwa kuzingatia uadilifu, na kuisimaia misingi ya katiba na sheria za nchi. kwani kufanya hivyo, italinda haki za mtu binafsi na kujenga imani kwa jamii juu ya Muhimili wa Mahkma.\r\nAmeyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo Majaji na Mahakimu kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya Uchaguzi katika hoteli ya The dream of Sau inn Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja. \r\n\r\nAidha Mhe. Jaji Mkuu amesema kipindi cha Uchaguzi ni cha mpito ni wajibu wa Jaji au Hakimu kusimamia utoaji wa haki bila upendeleo kwa kuzingatia sheria, kanuni, na maadili ili kuleta amani itakayodumu kwa kipindi kirefu kwa wananchi wote wa Zanzibar.\r\nAkitoa salumu za Tume ya Uchaguzi wa Zanzibar katika Mafunzo hayo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji George Kazi amesema Tume inaendesha uchaguzi huru na wa haki kwa mujibu wa sheria zilizopo bila ya upendeleo wa chama chochote cha siasa.\r\n\r\nKwa upande wake mkurugenzi Mkuu wa shirika la maendeleo endelevu na Democrasia Barani Afrika Antoneta Hamandishe amesema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha kuelekea kipindi hiki cha uchaguzi Migogoro ya kiuchaguuzi inatatuliwa kwa kuzingatia Sheria,Taratibu,na Miongozo iliyopo kulingana na katiba ya Zanzibar n jamhuri ya Muungano wa Tanzania.\r\n\r\nMafunzo hayo ya siku mbili yameandaliwa na Mahakama ya ya Zanzibar kwa kushirikiana na Shirika la Eisa lenye makao makuu yake Nchini South Afrika Kwa Ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uingereza (FCDO).