Skip to main content

New e-CMS system launching February 1, 2026 | Learn more

JAJI MKUU AZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI WA MAHKAMA

2025-10-04 Zanzibar Judiciary
Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Khamis Ramadhan Abadalla amewasisitiza wafanyakazi wa Mahkama kufanya kazi kwa uwadilifu na kuwa na maneno mazuri katika kuwahudumia wananchi wanapokwenda kwenye Majengo ya Mahkama kupata huduma. \r\n\r\nAmeyasema hayo wakati wa Ziara yake ya kuzungumza na wafanyakazi wa Mhakama ya Mkoa wa Mjini Magharib Mazizini na Mahkama ya Wilaya ya Magharib B iliyopo kisakasaka.\r\n\r\nAidha amesema uzuri wa Majengo ya Mahkama unapaswa kwenda sambamba na huduma bora zinazotolewa kwa wanachi wanaohitaji huduma za Mahkama na kuwa Mashauri yaliyokuwa Mahkamani yanasikilizwa na kutolewa uamuzi kwa wakati.\r\n\r\nVile vile Mhe. Jaji Mkuu aliwakumbusha wafanyakazi wa Mahkama kujiepusha na viashiria vyovyote vile vya rushwa wakati wa kuwahudumikia wananchi kwani Uongozi wa Mahkama hautokuwa na muhali kwa mtumishi yoyote atakaebainika kuomba na kupokea rushwa katika kutekeleza majukumu yake ya kazi hatua kali za nidhamu zitachukuliwa dhidi yake.\r\n\r\nPia Mhe. Jaji Mkuu aliwakumbusha watendaji kuwa kwa sasa Taifa linaelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa Nchi, hivyo aliwaasa watumishi wa Mahkama kutoshabikia upande wowote wa chama cha siasa wanapokuwa kwenye Majengo ya Mahkama, wanapaswa kuwahudumikia wafuasi wa vyama vyote vya siasa kwa usawa. \r\n “ tufanye kazi kama wafanyakazi wa Taasisi hii muhimu sana bila ya kuingilia michakato ya Uchagukuguzi hatutaki mfanyakazi wa Mahkama kuja kazini amevaa sara za chama chake kwenye Majengo yetu” Alisema Mhe. Jaji Mkuu.\r\n\r\nNae kwa upande Kaimu Mrajis wa Mahkama Kuu Zanzibar Mhe. Faraji Shomar Juma aliwataka wafanyakazi hao kwa sasa kufanya kazi kwa bidii ili wananchi waone faida ya kuwepo kwa Majengo Mapya ya Mahkama. \r\n\r\nAidha alimshukuru Mhe. Jaji Mkuu kwa uongozi wake uliotukuka hali ambayo inaifanya Mahkama kupiga hatua kiutendaji. \r\n\r\nNao Wafanyakazi wa Mahkama wameshukuru Rais wa Zanzabar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi pamoja na Jaji Mkuu kwa Uongozi wao na kuona haja ya kuwajengea Majengo Mapya ya Mahkama za Mikoa na Wilaya\r\n\r\nAidha wafanyakazi wa Mahkama hizo waliuomba Uongozi wa Mahkama kuwaptia mafunzo ya mara kwa mara ili kuweza kuongeza ufanisi wakati wa kutekeleza majukumu yao.